1 Chronicles 26:4-10

4Obed-Edomu naye alikuwa na wana wafuatao:
Shemaya mzaliwa wa kwanza,
Yehozabadi wa pili,
Yoa wa tatu,
Sakari wa nne,
Nethaneli wa tano,
5 aAmieli wa sita,
Isakari wa saba,
na Peulethai wa nane.
(Kwa kuwa Mungu alikuwa amembariki Obed-Edomu.)

6Shemaya mwanawe pia alikuwa na wana, waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa. 7Wana wa Shemaya ni: Othni, Refaeli, Obedi na Elizabadi; jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa pia watu wenye uwezo. 8Hawa wote walikuwa wazao wa Obed-Edomu; wao na wana wao na jamaa zao walikuwa watu wenye uwezo pamoja na nguvu za kufanya kazi. Wazao wa Obed-Edomu jumla yao walikuwa sitini na wawili.
9Meshelemia alikuwa na wana na jamaa zake, waliokuwa watu wenye uwezo: jumla yao watu kumi na wanane.

10 bHosa, Mmerari, alikuwa na wana wafuatao: Shimri alikuwa mkuu wao (baba yake alikuwa amemweka yeye kuwa mkuu ijapokuwa hakuwa mzaliwa wa kwanza),
Copyright information for SwhNEN